Malengo
LENGO KUU
- Kukusanya, kuweka kumbukumbu, kuhifadhi na kuendeleza historia ya ukombozi wa Afrika iliyotokana na harakati za kupigania uhuru.
MALENGO MAHSUSI
- Kuamsha na kuendeleza utafiti wa urithi wa ukombozi wa Afrika;
- Kulinda, kuhifadhi na kuendeleza Urithi wa Ukombozi wa Afrika;
- Kuanzisha mfumo wa kuenzi mashujaa na kuendeleza umiliki wa urithi wa ukombozi wa Afrika;
- Kujenga uwezo wa kitaalamu katika kusimamia na kueneza urithi wa ukombozi wa Afrika;
- Kuratibu Programu hii kwa ushirikiano miongoni mwa Nchi Wanachama wa Programu hii; na
- Kutangaza maeneo ya urithi wa ukombozi katika gazeti la Serikali ili yalindwe kisheria.