Michikichi

MICHIKICHI AINA YA TENERA

SIFA

  1. Miche hii ya kisasa ya michikichi huanza kuzaa baada ya miaka mitatu (3).
  2. Mashudu yake hutumika kama chakula cha wanyama.
  3. Mche mmoja hutoa lita 28 za mafuta kwa mwaka.
  4. Inatoa kiasi cha lita 5600 za mafuta kwa hekari.
  5. Mafuta yake yana wingi wa vitamini A.
  6. Kokwa hutumika kutengeneza sabuni.
  7. Matawi hutumika kama mifagio na kuezeka nyumba.
  8. Mti wake hutumika kukata mbao.

NAFASI KATIKA UPANDAJI

Nafasi ya kupanda ni mita 9 kati ya shimo na shimo na nafasi kati ya mstari na mstari ni mita 7.8. Kwa nafasi hizi, utapata miti 142 kwa hekari.

PALIZI

Kwa kutumia njia ya mkono, miti ya michikichi hupaliliwa kwa kutengeneza visahani kuzuguka shina la mchikichi.Visahani hivi huwa ni vya upana wa mita moja (1) kutoka kwenye shina kwa mimea michanga na upana wa mita mbili (2) kutoka kwenye shina kwa mimea mikubwa.

Katika njia ya dawa, dawa ipulizwe kuzunguka shina la mchikichi kwa upana uliotajwa hapo juu na isipulizwe kwenye mti ili kuepusha kuunguza.

MATUMIZI YA MBOLEA

Michikichi inahitaji mbolea nyingi iweze kustawi vizuri na kuzaa sana.

Mbolea ya kupandia inayoshauriwa kutumika ni Samadi kwa wingi wa debe moja (1) kwa shina

Mbolea ya kukuzia inayoshauriwa kutumika ni UREA au CAN

MAGONJWA NA WADUDU WANAOSHAMBULIA MICHIKICKI NA UDHIBITI

1. MAGONJWA

 1 (a) Fangasi

S/N Ugonjwa Udhibiti
1 Kuoza kwa vitako (Ganoderma butt rot)
  •  Kung'oa na kuchoma miti iliyoathirika.
  •  Isipandwe mimea mipya katika udongo ambao uling'oa miti iliyoathirika.
2 Mnyauko (Oil palm wilt)

Weka karantini sehemu zenye ugonjwa

Miti inayoonesha dalili ing'olewe na kuchomwa

Udongo ambao imeng'olewa mimea iliyokua na ugonjwa  iwekwe dawa ya Dazomet na kufunikwa kwa muda wa siku 30 kabla ya kupanda miti mingine.

 

 1 (b) Bacteria

Ugonjwa Udhibiti
Baka jani (Pestalotiopsis leaf spot)
  • Miti iliyougua kabisa iondolewe shambani na kuchomwa moto
  • Miche ipandwe kwa nafasi zinazotakiwa ili kuruhusu hewa kupita
  • Palilia mara kwa mara kuondoa magugu

 

2. WADUDU

S/N Wadudu Udhibiti
1

Wadudu wanaovyonza

  • Vidung'ata (Mealybugs)
  • Vidukari (Aphids)
  • Vidugamba (Scales)
Wadudu wote hawa hudhibitiwa kwa kupuliza kemikali kwenye majani ambazo zina viambato vya Dimethoate au Acephate. Viko kwenye dawa kama vile Rogo, Actellic, Selecron na Dursaban.
2 Viwavi (Caterpillars) Kupulizia kemikali zenye viambato vya BTK.
3 Wadudu Chonga (Rhinoceron beetle)
  • Fanya usafi shambani kwa kutoa maozea ya machina ya michikichi katika shamba ambalo ni mazalia ya wadudu hawa.
  • Kupulizia kemikali zenye viambato vya Phorate au Chloropyrifos