Nyanya
Nyanya
TANYA
SIFA
- Inafanya vizuri ukanda wa chini mpaka nyanda za juu kusini (0 - 1700)
- Ni rahisi kuzalisha kwani haihitaji maegemeo kama miti, kamba n.k ikiwa shambani
- Huzaa mazao mengi hadi tani 16 - 24 (kilo 16,000 - 24,000) kwa hekari moja
- Huzaa matunda yenye ganda gumu hivyo kuweza kusafirishwa umbali mrefu bila kuharibika kirahisi
- Matunda hukaa muda mrefu siku 20 - 30 bila kuharibika hivyo ni nzuri kwa biashara
TENGERU 97
SIFA
- Inapendekezwa kulimwa ukanda wa kati mpaka wa juu (400 - 1500)
- Huzaa mazao mengi, tani 20 - 40 (kilo 20,000 - 40,000) kwa hekari moja
- Huvumilia magonjwa kama batobato (mozaic), minyoo fundo (roots nematods), mnyauko fusari (fusarium wilt)
- Huzaa matunda makubwa, mekundu, yenye umbo la mviringo na mazuri kwa kusindika