ASA YAENDELEA KUNUFAIKA NA MRADI WA AFDP KUPITIA PROGRAM YA IFAD

Mkurugenzi wa Maendeleo ya Biashara Wakala wa Mbegu za Kilimo ASA Bi.Mary Machaku akimwakilisha Mtendaji Mkuu (ASA) ameongoza timu ya wataalamu kutoka ASA na wasimamizi wa mradi kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu (PCU) kwaajili ya kukagua na kukabidhiwa kwa ASA kutoka kwa wakandarasi, miradi hii inayofadhiliwa na IFAD kupitia Program ya AFDP katika Shamba la Mbegu Kilimi-Nzega.
Miradi hii ni pamoja na ujenzi wa jengo la kukaushia mbegu (Drying Shade) na karakana ambayo yamekamilika kwa asilimia 100 na kugharimu jumla ya fedha za kitanzania shilingi milioni 248.124 ambapo kwa sasa majengo hayo yapo tayari kwa kuanza kutumika.
Bi, Mary Machaku amewapongeza wahandisi wa Wakala wa Mbegu ASA kwa kusimamia miradi mbalimbali inayotolewa na Serikali kwa Wakala ambayo inasaidia kutatua changamoto mbalimbali ikiwemo maeneo ya kukaushia mbegu, maghala ya kuhifadhia mbegu, mitambo ya kuchakata mbegu, pamoja na karakana kwaajili ya kukarabati zana za kilimo na mitambo ya kilimo.
Aidha, Mkurugenzi huyo ameishukuru Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya Rais wa awamu ya sita Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutoa fedha kwaajili ya Sekta ya Kilimo. Pia amemshukuru Waziri wa Kilimo Mhe. Hussein Bashe (Mb) kwa kuipambania Sekta ya kilimo na kuleta mageuzi makubwa ya kilimo hapa nchini.
Aidha, amemshukuru Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Bwana Gerald Mweli kwa kusimamia vema upatikanaji wa fedha kwaajili ya miradi na shughuli mbalimbali za kilimo. Aliendelea kutoa shukurani zake kwa kumshukuru Mkurugenzi Mtendaji wa ASA Bwana Leo Mavika kwa jitihada zake za kuhakikisha fedha zote zinazotolewa na Serikali zinatumika kama zinavyokusudiwa.
Pamoja na shughuli ya kupokea miradi mwili iliyo kamilika, pia Bi Mary Machaku aliongoza timu hiyo kumkabidhi Mkandarasi Bwana Honest Uiso mwenye kampuni ya Namis Corporate Ltd eneo la ujenzi wa nyumba za watumishi katika shamba la Mbegu Kilimi.
Kwa Mujibu wa Mkataba Mkandarasi huyo anapawa kujenga nyumba mbili za watumishi kwa mtindo wa nyumba mbili kwa moja (2IN1) zitakazoweza kuchukua familiya nne (4). Alimtaka Mkandarasi huyo kujenga nyumba hizo kwa kuzingatia ubora na viwango stahiki ili thamani ya fedha ionekane (value for money) na kumaliza kwa wakati kulingana na muda uliowekwa kwenye mkataba huku Ujenzi huo ukifadhiliwa na mradi wa AFDP.
[03/06/25, 08:17:20] Mfaume: https://www.instagram.com/p/DJbkRc4N45l/?igsh=MWNsOG02bzU0b3kzMA==
Wakala wa Mbegu za kilimo (ASA) yakabidhiwa Shamba la Mbegu za kilimo lenye Hekta 240 sawa na Ekari 601 kutoka Halmashauri ya wilaya ya Igunga kwa ajili ya kuzalisha Mbegu bora za kilimo.
Akizungumza na waandishi wa Habari Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Igunga Bi. Selwa Abdalah amesema Baraza la Madiwani limeridhia kutoa shamba hilo lililokuwa likimilikiwa na Halmashauri ya Igunga.
“Hatua hii imefikia baada ya Waziri wa kilimo Mhe.Hussein Bashe akiwa katika ziara yake ya kikazi alitoa agizo kwa Halmashauri kutoa eneo la Uzalishaji wa Mbegu katika wilaya hiyo. Tayari Halmahshauri hiyo kupitia Baraza la Madiwani wametekeleza maagizo ya Waziri wa Kilimo kwa kutoa eneo lengo likiwa ni kuongeza Uzalishaji wa Mbegu na kupunguza muda na gharama za upatikanaji wa mbegu kwa wakulima wa Igunga, shamba hilo lipo katika Kijiji cha Bulyashiri kata ya Mwalala wilaya ya Igunga Mkoani Tabora. Amesema Bi. Selwa
Mkuu wa wilaya ya Igunga Bi. Sauda Mtondoo akikabidhi hati ya shamba hilo dhidi kwa Wakala wa Mbegu za kilimo ASA amesema, serikali ya Igunga itahakikisha inatoa ushirikiano wa kutosha kwa Wakala wa Mbegu katika hatua mbalimbali za Uzalishaji wa Mbegu.
Kwa upande wake Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Mbegu za kilimo ASA Bwa. Leo Mavika ameipongeza Halmashauri ya wilaya ya Igunga kwa kutenga eneo hilo la Uzalishaji wa Mbegu Hekta 240.
“Shamba hili litawekewa miundombinu ya Umwagiliaji na kufungwa mitambo mbalimbali ya kisasa ya kuchakata Mbegu bora za kilimo tayari kuwafikia wananchi wa Igunga na Tanzania kwa Ujumla, pia litaongeza upatikanaji wa ajira mbalimbali kwa wananchi shambani na urahisi wa upatikanaji wa Mbegu pamoja na baadhi ya wakulima wanaolima jirani kupewa Mbegu bure kwa ajili ya kulinda ubora wa Mbegu. Amesema Bwa. Leo
Akimwakilisha Katibu Mkuu Wizara ya kilimo Mhandisi.Juma Mdeke amesema wizara ya kilimo imeishukuru Halmashauri ya Igunga kwa kukabidhi shamba hilo kwa ASA ambapo matarajio ni kuleta mchango mkubwa katika upatikanaji wa mbegu nchini.