Majukumu
- Kutambua, kuhifadhi, kulinda, kuendeleza, kurithisha, kutangaza maeneo ya Ukombozi wa Afrika pamoja na kukusanya nyaraka zilizopo nchini;
- Kuratibu na kusimamia uanzishwaji wa Kituo cha Urithi wa Ukombozi wa Afrika Dar es Salaam-Tanzania;
- Kuratibu tafiti, kuchapisha na kutangaza taarifa za utafiti kuhusu Urithi wa Ukombozi wa Afrika kwa kushirikiana na wadau na wanataaluma;
- Kuandaa sheria, kanuni na miongozo ya kulinda, kuhifadhi na kuendeleza Urithi wa Ukombozi wa Afrika;