Tanzania emblem

Programu ya Urithi wa Ukombozi wa Afrika

Urithi wa Ukombozi, Fahari ya Afrika

Programu ya Urithi wa Ukombozi wa Afrika

Habari

Ziara chuo cha Mifugo na Kilimo, Kaole Bagamoyo.


Matukio katika picha wakati Mratibu wa Kituo cha urithi wa ukombozi Afrika Bw. Christopher Mhongole pamoja na maafisa wa Kituo walipotembelea Chuo cha Mifugo na Kilimo cha Kaole Agosti 25, 2025.

Mwanzoni mwa miaka ya 1960, chuo hiki kilitumika kama kambi ya kijeshi kwa wapigania uhuru kutoka nchi mbalimbali za kusini mwa Afrika ikiwemo wapigania uhuru kutoka Zimbabwe, Rais wa Zimbabwe, Emmerson Mnangagwa, ni miongoni mwa waliopata mafunzo katika chuo hicho na amewahi kuthibitisha kuwa Kaole ilikuwa sehemu muhimu ya maandalizi ya wapigania uhuru wa Zimbabwe, Afrika Kusini na Msumbiji. Baada ya harakati za ukombozi kambi hii ilibadilishwa na kuwa Chuo cha Mifugo na Kilimo, lakini bado kinahifadhi historia ya mchango wake katika ukombozi wa Afrika.