Habari
Jamii yaelimishwa kuhusu utekelezaji wa majukumu ya Kituo cha Urithi wa Ukombozi wa Afrika
19 Desemba, 2025 – Dar es Salaam
Kituo cha Urithi wa Ukombozi wa Afrika kimetoa elimu kwa jamii leo tarehe 19 Desemba, 2025 kupitia StarTV na Kiss FM Redio ili kuelezea majukumu yake na kuhamasisha utalii wa kihistoria nchini. Hii ni sehemu ya programu ya kueneza uelewa kuhusu urithi wa ukombozi wa Afrika kwa jamii hususani vijana.
Akizungumza katika vipindi vya Kivuko na Morning Kiss vinavyorushwa na StartTV na Kiss FM, Mratibu wa Kituo, Bw. Christopher Mhongole, alisisitiza umuhimu wa Kituo katika kuhifadhi na kuendeleza historia ya harakati za ukombozi, akieleza kuwa Tanzania ni kitovu cha urithi huu muhimu kwa Afrika.
Katika mahojiano, alisema, "Kituo hiki ni hazina ya maarifa na urithi kwa Watanzania na Waafrika wote, na tunahakikisha historia ya ukombozi haipotei, na ndio maana kwa kulitambua hilo Mawaziri wanaoshughulikia masuala ya Vijana, Utamaduni na Michezo wa Umoja wa Afrika waliazimia Kituo kiwe taasisi inayosimamiwa na Umoja wa Afrika katika Mkutano uliofanyika Bujumbura Burundi tarehe 8–13 Desemba, 2025."
Fuatilia zaidi Kipindi cha Kivuko cha StarTV tarehe 22 Desemba, 2025, saa 3:00 Usiku na Morning Kiss cha Kiss FM saa 2:00 Asubuhi siku ya Jumanne.

