Habari
Ziara Mashuleni
Kituo cha Urithi wa Ukombozi wa Afrika kimefanya ziara maalum katika shule ya sekondari Juhudi, iliyopo wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam. Ziara hiyo ni sehemu ya programu endelevu ya kituo inayolenga kuwafundisha wanafunzi kuhusu historia na harakati za ukombozi barani Afrika.
Kupitia mijadala na maonesho wanafunzi walipata fursa ya kujifunza kuhusu viongozi wa harakati za ukombozi na umuhimu wa kuhifadhi urithi wa kihistoria kwa vizazi vijavyo.

