BODI YAWASIHI WATUMISHI ASA KUFANYA KAZI KWA BIDII NA UBUNIFU ILI KUONGEZA UZALISHAJI WENYE TIJA
19 Mar, 2025
BODI YAWASIHI WATUMISHI ASA KUFANYA KAZI KWA BIDII NA UBUNIFU ILI KUONGEZA UZALISHAJI WENYE TIJA

Bodi ya Ushauri ya Wakala wa Mbegu za kilimo (ASA), yawasihi watumishi wa ASA kufanya kazi wa bidi na kuongeza ubunifu katika kazi ili kuongeza uzalishaji wa mbegu bora za kilimo nchini. 

Akizungumza na watumishi hao  Jumatatu  Machi 17, 2025 Makao makuu ya ASA jijini Morogoro mwenyekiti wa Bodi ya Washauri ASA, Bi. Mary  Kipeja amewataka watumishi wote wa ASA kufanya kazi kwa kujituma na kuongeza ubunifu pia kuwajibika katika nafasi yake ili kuongeza ufanisi wa kazi.

"Lazima wote tufanye kazi kwa pamoja tujitume ili tuongeze Uzalishaji wa Mbegu ambao kwa sasa bado mahitaji ni makubwa nchini, tunapaswa kujiendesha kwa faida huku ikiongeza uzalishaji wa mbegu na usambazaji kwa wananchi kwa bei nafuu pia tuwe na mtazamo chanya wenye mabadiliko ya kiuchumi kwa Taasisi nakuongeza mapato" Bi Kipeja.


Kwa upande wake Bi, Shamira Mshangama Mjumbe wa Bodi hiyo amesema Wakala wa Mbegu ASA inapaswa kuongeza mapato yake na kupunguza matumizi yasiyo ya  lazima hivyo kuna kila sababu ya watumishi kufanya kazi vizuri na kupunguza matumizi.

“Sisi kama Bodi tunaahidi kushirikiana na  watumishi kwa kutatua changamoto mbalimbali tulizoziona na kuondoa vikwazo vya kushindwa kufanya kazi.” Bi, Mshangama

Aidha kwa upande wake Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Mbegu za kilimo ASA Bwa. Leo Mavika ameipongeza bodi hiyo kwa kuanza kazi na kufanya ziara ya kukagua Mashamba na kuona changamoto na mafanikio ya Wakala katika sekta ya Uzalishaji wa Mbegu za kilimo.

“Wakala itashirikiana na Bodi hiyo kwa muda wote ili kuhakikisha ASA inapata mafanikio hasa kuongeza Uzalishaji wa Mbegu na usambazaji nchini”
 

Pia bodi hii ilipata wasaa wa kuhidhinisha rasimu ya bujeti ya Wakala kwa mwaka 2025/2026 na kuipongeza taasisi kushirikisha meaneo yote muhimu katika Uzalishaji wa mbegu bora za kilimo na kuongeza Uzalishaji wenye tija.