ASA YATOA FURSA KWA WAFANYA BIASHARA WA MBEGU ZA KILIMO.
ASA YATOA FURSA KWA WAFANYA BIASHARA WA MBEGU.
Wakala wa Mbegu za kilimo ASA imetoa fursa kwa mawakala wa uuzaji wa Mbegu za kilimo kushirikiana na Taasisi hiyo Kwa kuuza Mbegu.
Akifungua Kikao Cha Mawakala wa uuzaji wa Mbegu pamoja na Maafisa kilimo wa Halmashauri 56 kilichofanyika October 16 Mkoani Morogoro Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Mbegu za kilimo ASA Bwn,Leo Mavika amesema ASA imetoa fursa kwa wafanya biashara wa Mbegu kuuza Mbegu bora za ASA.
Amesema mipango ya ASA ni kupata mawakala waaminifu ambao watauza Mbegu hizo ili ASA ibaki na jukumu moja la kuzalisha wa Mbegu.
Bwn Mavika akifafanua mpango kazi wa Taasisi amesema, lengo ni kuwa na mawakala wakubwa wachache ambao watasambaza mbegu hizo kwa mawakala wa kati kisha mbegu hizo kuwafikia wakulima kwa bei nafuu.
Aidha Kaimu Mtendaji Mkuu amewaomba mawakala hao kutoa ushirikiano wakutosha wa kuhakikisha wanafanya kazi kwa pamoja na ASA ili kuweza kuwafikia wakulima kwa haraka na urahisi.
Amesema mbegu za ASA ni nzuri na zimeandaliwa kwa kufuata utaratibu madhubuti wa kisheria wa uzalishaji chini ya Taasisi ya uzibiti bora wa Mbegu (TOSCI).
Kwa upande wake Meneja Afisa Masoko wa Wakala wa Mbegu za kilimo ASA Edward Mbugi amewataka mawakala hao kuwa waaminifu katika kuhakikisha mbegu za ASA zinauzwa vizuri.
Amesema baadhi ya mawakala wamekuwa sio waaminifu kwa kuchafua soko la Mbegu za Wakala pamoja na kushindwa kulipa madeni yao kwa wakati.
Meneja Masoko amesema changamoto zote zilizo tokea kwa Wakala zitafanyiwa kazi haraka kulingana na uzito wake ili mambo yote yaweze kwenda vizuri kama ilivyopangwa.
Baadhi ya Maafisa kilimo wa Halmashauri waliohudhuria Kikao hicho wametakiwa kutoa ushirikiano kwa Wakala ilikuhakikisha Mbegu za Wakala zinawafikia wakulima kupitia mawakala.
Wameipongeza ASA kwa kuwashirikisha katika Kikao hicho muhimu Cha kujenga na kuboresha mikakati ya Wakala ili iweze kuwafikia wakulima Kwa urahisi.
Mwisho.