WATUMISHI WA ASA WAPATA MAFUNZO YA TEKINOLOJIA YA UZALISHAJI WA MBEGU BORA ZA KILIMO.
Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Mbegu za kilimo (ASA) Bw. Leo Mavika amewataka Maafisa Kilimo wa Wakala wa Mbegu za kilimo kuhakikisha wanaongeza Uzalishaji wa Mbegu bora za kilimo ili kuweza kufikia Malengo yaliyowekwa na serikali.
Amesema hayo wakati akifungua Mafunzo ya Siku Tatu ya Technolojia za Uzalishaji wa Mbegu bora za kilimo kwa maafisa kilimo wa ASA Mkoani Dodoma yanayotekelezwa kupitia programu ya kuendeleza kilimo na Uvuvi - AFDP.
Amesema watumishi wote waliohudhuria Mafunzo hayo wanapaswa kuzingatia Elimu itakayotolewa na wataalam ili kuleta ufanisi kwenye mashamba ya Taasisi.
Amesema ASA inajukumu kubwa la kuhakikisha inazalisha Mbegu bora Kwa wingi ili kukidhi mahitaji ya Nchi na kuepuka kuagiza Mbegu za kilimo kutoka Nje ya Nchi.
Amesema Wakala wa Mbegu za kilimo ASA ina kipaumbele cha kuzalisha mbegu za Mazao 13 ambazo zinapaswa kupatikana wa wingi ikiwemo zao la Mahindi, Alizeti,Mpunga pamoja na Mazao mengine.
Kaimu Mtendaji Mkuu Mavika amesema Wakala wa Mbegu za kilimo ASA inatakiwa kuchangia kwa sehemu kubwa uzalishaji wa Tani 127,650 ambazo ndio mahitaji halisi ya Nchi.
Aidha amesama Malengo ya Taasisi ni kuona mabadiliko makubwa baada ya Mafunzo hayo katika Mashamba kutokana na kupewa Mafunzo bora ya Uzalishaji wa Mbegu kutoka kwa wataalamu waliobobea watakaowasilisha mada.
Bwn, Mavika amepongeza Mafunzo hayo yanayotekelezwakuoitia Programu ya kuendeleza kilimo na Uvuvi -AFDP na amesema yatasaidia kukuza uelewa kwa watumishi nakusaidia kuboresha uzalishaji na kufikia Malengo.
Aidha kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Biashara Emmanuel Maziku amesema progranu hiyo inatekeleza miradi mbalimbali kwenye Mashamba mawili ambayo ni Shamba la Kilimi Nzega pamoja na Shamba la Msimba Kilosa Mkoani Morogoro.
Amesema Miradi inayotekelezwa kupitia programu hii ni ujenzi na ukarabati wa karakana, Ofisi, nyumba za watumishi, ghala majengo ya ofisi, karakana, Ghala na maeneo ya kuanikia mbegu. aidha inawezesha ununuzi wa la kuhifadhia Mbegu Mtambo wa kuchakata Mbegu na zana za kilimo
Aidha amesema pamoja na uwekezaji huo, programu inawezesha kuongeza uzalishaji wa Mbegu Bora pamoja na kuhamasisha sekta Binafsi kushiriki kuzalisha Mbegu bora za kilimo.