ASA YAKABIDHI KILO 490 ZA MBEGU ZA MSINGI KWA WAKULIMA WADOGO 40
Wakala wa Mbegu za kilimo ASA imekabidhi kilo 490 za Mbegu za msingi kwa wakulima wadogo wazalishaji wa Mbegu daraja la kuazimiwa ubora ikijulikana pia kama Umbegu (QDS) .
Akifunga Mafunzo ya Tekinolojia za Uzalishaji wa Mbegu za kilimo yaliyo fanyika katika ukumbi wa Romani complex Mkoani Dodoma Mkurugenzi wa Biashara Bi, Mery Machaku amewataka wakulima hao kwenda kuzalisha Mbegu bora za kilimo kama walivyo fundishwa.
Amesema Wakala wa Mbegu za kilimo ASA umetoa Mbegu hizo kwa lengo la kuwawezesha wakulima hao kuwa na Mbegu bora watakazoanza kuzalisha kwa msimu wa kilimo unaoendelea.
Mbegu walizopewa wakulima hao ni pamoja na mbegu za Alizeti aina ya Record kilo 68, Mahindi aina ya T105 kilo 298 , Maharagwe kilo80 pamoja na Mbaazi kilo 6.
Aidha amewata kuzalisha Mbegu hizo kwa kufuata taratibu na kanuni za Uzalishaji wa Mbegu kama walivyofundiwa na wataalamu wa Kilimo kutoa ASA,TARI pamoja na TOSCI.
Kwaupande wake Mtaalamu wa Ubora wa Mbegu wa Wakala wa Mbegu za kilimo ASA Bi, Grace Matina amesema wakulima hao wamepewa Mafunzo muhimu ya Uzalishaji wa Mbegu pamoja na kuhifadhi wa Mbegu hizo ili zisiharibike.
Amesema imani ya Wakala ni kuona wakulima wote 40 wanakuwa wazalishaji wa Mbegu bora za kilimo katika maeneo yao wanayotoka.
Mratibu wa programu ya AFDP Bi, Rozalia Mtenga amesema moja ya kazi zinazotekelezwa kupitia programu hiyo ni kuwezesha wazalishaji wa mbegu kwa mfumo wa QDS ili waweze kuzalisha na kuongeza upatikanaji wa mbegu kwenye maeneo ya programu.
"kutumia vizuri waliopata kuongeza uzalishaji wa mbegu na kujiinua kiuchumi kwani mahitaji ya mbegu ni makubwa na yanahitaji nguvu ya pamoja kuyatosheleza."