ASA NA BENKI YA CRDB WAKUTANA KUJADILI JINSI YA KUSHIRIKIANA KATIKA KUENDELEZA NA KUONGEZA UZALISHAJI WA MBEGU BORA ZA KILIMO.
ASA NA BENKI YA CRDB WAKUTANA KUJADILI JINSI YA KUSHIRIKIANA KATIKA KUENDELEZA NA KUONGEZA UZALISHAJI WA MBEGU BORA ZA KILIMO.
28 Mar, 2025

Wakala wa Mbegu za Kilimo (ASA) leo Machi 27, 2025 umepokea ujumbe kutoka banki ya CRDB katika ofisi zake zilizopo mtaa wa magodoro mjini Morogoro.
Katika kikao hicho wamezungumza mambo mbalimbali yanayolenga kuendeleza ushirikiano katika uzalishaji, uchakataji na usambazaji wa mbegu bora za kilimo kwa wakulima nchini.
Hii ni ishara ya dhamira ya Taasisi zote mbili ya kukuza mahusiano yenye tija katika Sekta ya mbegu, ikiwemo uzalishaji na uchakataji wa mbegu, pia Taasisi zote hizi zimejadili katika kuwekeza kwenye ujenzi wa maghala, Zana za kilimo, ununuzi wa mtambo ya kuchakata na kuanikia mbegu pamoja na mafunzo kwa wakulima wadogo wa mkataba