Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Mbegu za Kilimo (ASA) atoa mwelekeo mpya wa ASA
Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Mbegu za Kilimo {ASA} Bwn, Leo Justine Mavika ametoa Mwelekeo wa Taasisi hiyo ya Uzalishaji wa Mbegu Nchini kwa watumishi wa makao makuu Pamoja na wasimamizi wa Mashamba ili kujua mwelekeo wake.
Akizungumza na watumishi hao Mkoani Morogoro Kaimu Mtendaji Mkuu Leo Mavika amesema Mwelekeo wake ni kuongeza uzalishaji wa Mbegu Nchini ili kukidhi mahitaji ya Nchi na kupunguza kasi ya kuagiza mbegu kutoka Nchi za Nje.
Mavika amesema ASA ina wajibu wa
Kuongeza uzalishaji wa Mbegu na usambazaji wa mbegu bora Pamoja na Kuhamasisha sekta binafsi kushiriki katika uzalishaji kama mmoja ya jukumu la wakala wa mbegu kufanya kazi Pamoja na sekta binafsi.
Amesema licha ya kushirikiana na sekta binafsi katika uzalishaji wa mbegu ASA inatoa fursa kwa wafanya biashara kusambaza mbegu kwa wananchi ili ziweze kuwafikia kwa haraka.
Aidha Amesema wakala inawajibu wa kuhamasisha wananchi kutumia Mbegu bora za kilimo kupita matangazo mbalimbali lengo ni kumfikishia mkulima mbegu bora na kwa bei nafuu.
Amesea Wakala wa Mbegu za Kilimo ASA itaendelea kushirikiana na Taasisi za Wizara ya kilimo hasa Taasisi za utafiti (TARI) ili kuhakikisha mbegu mpya zinazalishwa na kukidhi mahitaji ya wakulima.
Akitaja Mahitaji ya mbegu nchini Kaimu Mtendaji Mkuu Bwn,Leo Mavika amesema kwa sasa ni tani 127,650 kwa mwaka, ambapo uzalishaji wa mbegu kwenye mashamba ya Wakala wa Mbegu za Kilimo (ASA) mwaka 2021/2022 na 2022/2023 ni tani 3,173 na tani 3,549.
Amesema Kwa mwaka 2024/2025 Wakala imepangiwa kuzalisha Tani 8,568 lengo ni kuongeza uzalishaji kwa tija na kupunguza gharama za uzalishaji.
Kaimu Mtendaji Mkuu amesema Taasisi hiyo inazo fursa nyingi za kuiwezesha kukua na kutoa mchango mkubwa zaidi kwa sekta ya kilimo na Taifa kwa ujumla kutokana na kuweka mikakati madhubuti na kuhakikisha inatekelezwa kwa dhati hasa kwenye maeneo yote ambayo yatawezesha kuongeza uzalishaji na tija ya mbegu pamoja na kuongeza mapato ya Wakala na kupunguza gharama za uzalishaji na uendeshaji.
‘’ Taa sisi yetu inazo fursa nyingi sana za kuiwezesha kukua na kutoa mchango mkubwa zaidi kwa sekta ya kilimo na Taifa kwa ujumla, hii itatokea tu ikiwa tutaweka mikakati madhubuti na kuhakikisha tunaitekeleza kwa dhati hasa kwenye maeneo yote ambayo yatatuwezesha kuongeza uzalishaji na tija ya mbegu pamoja na kuongeza mapato ya Wakala na kupunguza gharama za uzalishaji na uendeshaji.’’ Alisema Kaimu Mtendaji Mkuu Leo Mavika.
Amesema utendaji kazi wa wakala katika kipindi hiki, utapaswa kujielekeza katika kutafakari na kutafsiri kwa kila jambo linalofanyika kama kweli lina changia moja kwa moja katika kuongeza uzalishaji na tija ya mbegu na kuongeza mapato na kupunguza gharama za uendeshaji/uzalishaji.
Hata hivyo amesema Watumishi wote wa Wakala watapaswa kubadili mtazamo wao na kufikiri kibiashara zaidi (Business oriented mind).
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Wakala Dkt, Ashura Kihupi amepongeza hatua hiyo aliyoanza kuchukua Kaimu Mtendaji Mkuu Bwn, Leo Mavika ya kuanza kuzungumza na wakuu wa mashamba sambamba na kutoa mwelekeo wake wa Wakala.
Mweneyekiti huyo amesema suala la kuongeza uzalishaji wa mbegu na kupunguza gharama za uzalishaji ni miongoni mwa mambo ya msingi yanayotakiwa kufanyiwa kazi ilikuongeza uzalishaji wa mbegu nchini.
Dkt, Kihupi amewataka watumishi wote wa wakala wa Mbegu kutoa ushirikiano wa kutosha kwa Mtendaji huyo iliaweze kufanya kazi vizuri Pamoja na kuleta mabadiliko Chanya kwenye sekta hiyo ya kilimo.
Aidha alisema matarajio ya wajumbe wa Bodi nikuiona wakala ikifanya vizuri katika misimu yote ya uzalishaji wa mbegu.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Maendeleo ya Biashara Bi, Mary Machaku amesema wamepokea maelekezo yote na tayari wameanza kuyafanyia kazi kulingana na umuhimu wake kuelekea msimu wa kilimo 2024/2025.
Amewataka watumishi wote wa wakala kubadili mitazamo yao nakufuata maelekezo mapya yenye lengo la kuongeza uzalishaji wa mbegu kwa kupunguza gharama